Habari ya mjini ni Irene Uwoya na mtoto wa Ngarenaro dogo janja
Eliezer Gibson



Unaambiwa eti sismizi kambeba tembo,wengine lililomshinda ndikumana na Msami dogo kalibeba,yote ilimradi kila mtu anajaribu kutoa maoni juu ya inayotajwa kuwa ndoa ya star wa filamu na msanii kutoka Tip top dogo janja.
Ilianza dogo janja kusema anavutiwa na irene uwoya tangu kitambo,ikaja irene uwoya akaulizwa eti dogo anampenda akacheka na kusema yani kale(akimaanisha katoto). Mara tetesi zikaja eti wanadate mara paaap eti dogo janja amebeba mzigo jumla?
Tetesi zimezagaa kote kuwa moja kati ya A-list movie star wa kike Irene kafunga ndoa na mtoto wa Ngarenaro dogo janja japo mpaka sasa si irene au dogo janja aliyetoka hadharani na kukiri ukweli wa rumours hizo.
Kuna wengine wanasema dogo janja zugia tu ila kuna mwenye mwali wake kachill pembeni na wengine wanasema pengine nyimbo,lakini wengine wamekaza kukubali wanasema hii movie tu dogo hawezi chukua huu mzigo.
Wishes kutoka kwa mastar wenzao zimeongeza uzito kuwa pengine kweli dogo janja kaokota dodo kwenye muarobaini,sie yetu macho tunasubiri kwa hamu kuona yaliyomo yamo au kiki tu.
No comments