Story hii ya Leicester city ikupe Nguvu ya kuamini kudharauliwa Kwao sio sababu ya wewe kukata tamaa
Eliezer Gibson

Msimu wa wa ligi kuu ya EPL 2015/2016 ulianza kwa timu ya Leicester city kuwekwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kushuka daraja. Wachambuzi na wataalamu wa soka kote duniani waliona kushuka daraja ilikua ndo kitu kinachowezekana zaidi kwa Leicester kuliko kitu chochote kile.
Mwiso mwa msimu wote tunajua sio tu hawakushuka daraja bali walikua ni mabingwa wa ligi kuu ya soka Uingereza,mbele ya Mancity,man united,Chelsea,liver pool na Arsenal.maajabu yalioyoje duniani.
Katika maisha ya kawaida kuna watu tunafanya vitu na wala hatuonekani kama tunaweza kufikia lengo,wala hatuonekani kama tunafanania kuwa wenye mafanikio.watabiri wa mambo wanatutabiria kufa masikini kulingana na sababu wanazozijua wao,kulingana na nadharia walizozijenga juu yetu.
Lakini nakwambia hiyo kwako ni silaha na wala sio ya kukuangamiza ila ya kukufanya uinuke na usonge mbele,muda mzuri wa kushida ni muda ule ambao wengine hawaamini kama utashinda ni muda ambao wengine wanakuona kama upo upo tu huo ndo muda wa kutulia na kufanya lile linawozekana.
Kama wataalamu wanaonekana kuwa ni wa soka hawakuona ubingwa wa Leicester city ukija,Basi kumbe hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako na ushindi wako mwenyezi Mungu ameuandaa,inuka kapambane mawingu sio mwisho tena ila ni sehemu ya kuanzia.
No comments