MASTA WATATU WA YANGA KUIKOSA ST.LOUIS MECHI YA MARUDIANO

WACHEZAJI 20 KUIFUATA  ST. LOUIS KESHO
:-Chirwa, Kamusoko na Dante kubaki Dar.

-Kikosi cha Yanga Sc kinatarajia kusafiri kesho asubuhi kueleka Shelisheli tayari wa mchezo wa marejeano na wenyeji  St Louis Fc kwenye ligi ya mabingwa afrika mchezo ulipangwa  kuchezwa jumatano ijayo Stade Liete.

-Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema   jumla ya nyota 20 na viongozi 10 kati yao 8 kutoka benchi la ufundi na 2 viongozi wa kamati tendaji watasafiri asubuhi ya kesho  kupitia Nairobi tayari kwa mchezo wa siku ya jumatano.

"Maandalizi yote muhimu yamekwisha fanyika, timu imefanya mazoezi ya mwisho leo tayari kwa safari hiyo, kwenye kikosi nyota waliokuwa na majeraha ya muda mrefu kama Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu na Yohana Mkomola wataendelea  kukosekana hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha, kucheza ugenini kuna changamoto zake lakini tumejiandaa vizuri kwa sababu tushacheza nje mara nyingi hivyo hakuna hofu kati yetu."
Alisema Ten 

-Pia Dismas Ten amesema mchezaji Thabani Kamusoko ambaye amepona majeraha yake hivi karibuni na kuanza mazoezi mepesi pia ameondolewa kutoka orodha ya nyota ambao wangesafiri kueleka Shelisheli ili apate muda wa kujifua zaidi ili kurejesha makali yake, mchezaji Obrey Chirwa  naye hayumo kwenye orodha ya wachezaji watakaosafiri kwa sababu ya maumivu ya misuli aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Majiamaji.

"Ilikuwa asafiri  kueleka Shelisheli, lakini imelazimu benchi la ufundi kumuondoa kwa sababu bado hajawa ‘fit’ asilimia 100, anahitaji muda wa kujifua zaidi ili kupata utimamu wa mwili tayari kwa mapambano uwanjani, daktari wake pia amethibitisha kuwa mchezaji anatakiwa apate muda wa kujiweka sawa kabla hajaanza kucheza mechi kulingana na majeraha aliyokuwa nayo".

-Orodha kamili ya wachezaji ambao watasafiri kesho kuelekea Shelishelini kama Ifuatavyo: Makipa:- Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya, Youthe Rostand. Mabeki:- Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Gadiel Michael, Nadir Haroub Cannavaro, Patto Ngonyani, Kelvin Yondani, na Said Juma Makapu. Viungo:- Papy Tshishimbi, Pius Buswita, Raphael Daud, Yussuf Mhilu,  Said Mussa Bakari na Geoffrey Mwashiuya, Huku washambuliaji ni Juma Mahadhi, Emmanuel Martin na Ibrahim Ajib

Souurce: Yossima Sitta Jr.🙏🙏

No comments