BREAKING NEWS:TUME YA UCHAGUZI JIMBO LA SIHA LAMTANGAZA MSHINDI KITI CHA UBUNGE


Vyama mbali mbali vilikuwa katika kinyang'anyilo cha uchaguzi wa marudio katika Majimbo mawili Siha na Kinondoni ambapo leo hii ilikuwa ndio tamati ya ku amua nani aridhi mikoba.
 Muda huu nakusogezea Matokeo katika Jimbo la Siha ambapo Msimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro Valerian Juwal  amemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Dr. Godwin Molel kuwa mshindi katika uchaguzi wa Jimbo hilo uliofanyika February 17, 2018.
Dr. Molel amepata kura 25611 akifuatiwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Elvis Mosi aliyepata kura 5905 huku Mgombea wa Chama cha Wananchi CUF Tumsifuel Mwanri akipata kura 274 na wa Chama cha SAU yeye akipata kura 170.
Valerian ametangaza Dr.Godwin Molel kuwa Mbunge Mteule wa Siha kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Source:Millad Ayo

No comments