ALICHO KISEMA WAZIRI WA ELIMU JUU YA KIFO CHA MWANAFUNZI WA NIT

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba,serikali itagharamia na kusimamia mazishi ya Mwanafunzi Akwilima Akwiline wa chuo cha NIT, aliyeuawa kwa Risasi na Polisi waliokuwa wakidhibiti maandamano ya Chadema.

Waziri Ndalichako amevitaka vyombo vya Uchunguzi kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo,ili waliohusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

No comments