MZEE AKAMATWA KWA KUTOBOA BOMBA LA MAFUTA



Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania wanamshikilia Ndg. Samwel Nzagi Kilang'ani mwenye umri wa miaka 63 kwa tuhuma ya kutoboa Bomba la mafuta ya Dizeli la "Single Point Mooring" mali ya TPA na  kujiunganishia bomba lake la mafuta hadi kwenye nyumba yake ambako ameweka mantaki makubwa ambayo ameyachimbia chini. 

Kwa sasa Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa hatua za uchunguzi na sheria huku watuhumiwa wengine wakitafutwa.





No comments