MKUU WA MKOA AONGEA NA WANANCHI LIVE MASAA 3



Hu ni utaratibu alio jiwekea mkuu wa mkoa wa Mbeya kuweza kuongea na wanainchi wake katika ukumbi wa mkapa, Hutoa nafasi ya mara mbili kwa juma kama sehemu ya kusikiliza kero na changamoto za wakazi wa jiji la Mbeya.

Pia hutumia vituo vya radio kuongea na wanainchi walio shindwa kupata nafasi ya kumuona huongea nao moja kwa moja katika vipindi vya radio Wiki hii alitumia kituo cha Radio Ushindi kuongea na wanainchi wa Mbeya
Piaalisha fanya hvy katika vituo vya
Redio Dream Fm, Big Fm,  highland Fm, Bomba Fm
Pia ameahidi kuendelea kutembelea vituo kadha wa kadha vilivyo baki.

Amewahakikishia wananchi kuwa serikali itaendelea kutoa HUDUMA ya kiwango cha hali ya juu kwa wananchi wote na Anewataka watendaji kubadilika na kutoa huduma nzuri kwa wananchi ikiwemo kupunguza urasimu na kutatua kero za wananchi

Amewataka  wakuu wa wilaya,Wakurugenzi na maafisa kilimo kuhamasisha kilimo na kuwafikia wakulima. maafisa ugani ngazi ya kata na kijiji kuwajua wakulima,  mahitaji ya pembejeo, uratibu wa upatikanaji pembejeo,changamoto za wakulima na masoko ya MAZAO YA wakulima

Mkoa wa Mbeya unafanya vizuri kiuchumi kitaifa , mategemeo ni kufanya vizuri zaidi na amebainisha fursa nyingi zitajitokeza kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa meli mbili za mizigo ziwa nyasa na mara pia uwanja wa ndege wa songwe utakapokamilika fursa za utalii zitaongezeka na usafirishaji wa  mbogamboga matunda  na bidhaa zingine zitaongezeka

Kuhusu usalama amelitaka jeshi la POLISI kuimarisha usalama wa Raia na MALI zake na kupambana kwa nguvu zote na wahalifu 
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa.

No comments