ALIE JIFANYA WAKILI ANASWA
Jeremiah Ragita (Alie jifanya wakili)
Yaliyotokea leo Mahakama Kuu - Divisheni ya Ardhi Dsm
Munamo saa 6 mchana kulikuwa kuna kesi ya ardhi na 9 ya Mwaka 2017 ikiwainaendelea mbele ya mh Jaji Crecencia Makuru.
Bwana Jeremiah Ragita alijifanya kuwa wakili akitokea kampuni ya sheria ya Faithful Attorney Advocates akimsimamia mleta maombi Nunu Mhusin Mkwata. Upande wa pili ambao unasimamiwa na wakili Maros Gabriel kutoka kampuni ya sheria ya Common Law Chambers ulimtilia shaka bwana Jeremiah Ragita kama kweli ni wakili. Ndipo walipo amua kufanya upekuzi kwenye ofisi ya TLS na kuambiwa kuwa hawana jina Hilo.
Akaandika Barua Kwa RHC na kujibiwa kuwa hakuna wakili aliyesajiliwa Kwa jina hilo. Ndipo Leo Wakati wa kesi hiyo ilipoitwa Kwa mh Jaji Makuru, wakili Gabriel Maros alimueleza mh Jaji kuwa ana wasiwasi kuwa mwenzake wa upande wa pili siyo wakili. Akatoa vielelezo vyake kutoka Ofisi ya TLS na RHC.
Ndipo huyo wakili feki akakiri kuwa yeye si wakikili. Ndipo mh Jaji Makuru akaelekeza kuchukua hatua stahiki Kwa huyo mtu aliyejifanya wakili. Mhusika amewekwa kizuizini Kwa mahojiano zaidi.
No comments