Wenger na dunia ya kolasinac,psg na neymar

Kuna dunia ya PSG ambao wanaaminj soka kwa sasa linahitaji pesa ili uweze kufanikiwa kupata mafanikio,hii ndo dunia ambayo karibu kila mpenda soka na wadau wake wanaamini ndivyo inavyotakiwa iwe na wanajitahidi kwa kasi ya ajabu kufukuzana nayo.

Lakini kuna dunia ya Arsena wenger,pengine huyu yupo peke ake katika dunia hii,yeye bado anaamini uwekezaji wa pesa nyingi si njia sahihi ya timu kufikia mafanikio bado anaota kuwa ataweza kuleta mafanikio akiishi katika misingi yake aloanza nayo mwaka 96.

Wakati wa dirisha la usajili arsenal walisajili mlinzi wa kushoto kutoka schalke 04 anaitwa kolasinac ambaye alisajiliwa kwa uhamisho huru na mshambuliaji kutoka lyon lacazatte ambaye alisajiliwa kwa dau linalotajwa kufikia paundi 52.

Lakini dunia ambayo wenger anatamani wengine wote wawe wanaishi si dunia ya lacazzete,wenger anatamani kila mmoja aamini katika dunia ya kuweza kumpata mchezaji bure na akaleta impact kubwa kuliko hata mchezaji wa mamilioni.

Ukiangalia mwanzo wa maisha ya kolasinac unaweza kumuelewa wenger,katika mechi chache tu za msimu tayari ameonesha ni mchezaji wa nguvu assist mbili,magoli mawili,nguvu,kasi na spirit yake viko juu sana,kwa hakika unaona Arsenal imepata mtu.

Kwa bahati mbaya kupata huduma ya wachezaji kama kolasinac bure huwa inatokea mara moja tu katika maisha,dunia ya sasa ni ya kina mendy na walker kununuliwa kwa bei kubwa kuliko iliyomuhamisha zizou kutoka Juve kwenda real madrid hii sio dunia wenger anaitamani kuishi.


Ni wazi wenger ataendelea kuishi kwenye hii dunia ambayo ataendelea kubaki peke ake na ni dhahiri haiwezi kumpa mafanikio,ameokota dodo kwenye muarobaini kwa kolasinac lakini hawezi kuwa na bahati hiyo kila siku,siku hizi pesa zipo nyingi kuliko wachezaji atasubiri 

No comments