Unaishi ukiogopa maoni ya watu? Soma story hii ya sandra bullock utajifunza kitu
Eliezer Gibson
Kwa mwanadamu yoyote maoni na mawazo ya watu juu ya maisha yake hayaepukiki,ili mwanadamu aweze kuendelea haina budi kutega sikio kusikiliza kile watu wasemacho juu yake,japokua hatutakiwi tuishi kwa kufuata kila watu wanaloona na kusema juu yetu.
Marekani wana tunzo inaitwa Golden Raspberry Awards,Tunzo hii hutolewa kwa waigizaji waliofanya vibaya katika nafasi walizocheza kwenye filamu mbali mbali,sasa mwaka 2010 mwanadada sandra bullock alipewa tunzo hiyo kupitia filamu ya the blind side na tofauti na wengi wao yeye alikwenda na kupokea Tunzo hiyo.
Lakini cha kufurahisha ni kuwa kesho yake alipokea Tunzo ya mwigizaji bora wa kike kwenye filamu ile ile ya the blind side kupitia tunzo zingine za Academy award! Yani usiku mmoja ulitofautisha kupewa kama muigizaji bora na kama muigizaji mmbaya!
Ukiangalia kwa maisha ya kawaida utagundua kuwa,mtu unaweza ukafanya jambo fulani,kuna mwingine akaona ni la maana na mwingine akaona ni upuuuzi kama upuuzi mwingine tu,ko unafanyaje kama mwanadamu utaenda mbele ukifurahia sifa ulizopewa au utainama chini ukisikitika kwa kukosolewa kwako?
Kama mwanadamu jifunze kujitafakari wewe kwanza kabla hujampa nafasi mtu wa pili kukwambia nini cha kufanya,tengeneza mizani yako ya kupima yale unayoyafanya ili ujue njia ipi ya kwenda na ipi ya kutokwenda.
Jambo lolote utakalofanya litakua na pande mbili wanaokusifia na wanaokukosoa,ni vema ukayapa maoni yote ya pande mbili nafasi kisha ukachanganya na ya kwako ukasonga mbele kufuata lile linalokufaa,usiache mtu aaamue hatima yako,wewe ndo hakimu wa mwisho juu ya wapi unataka kufika.
Ni kweli kabisa. Naomba anitumie hii habari kwenye email yangu. Nimeipenda sana. Asubuhi njema... (23/10/2017)
ReplyDeleteSawa asante pia kwa kutembelea blog yetu endelea kuwa pamoja nasi
DeleteNmeipenda sana story hii,,, Tunashkuru na endeleeni kutupa mafunzo mengine zaidi
ReplyDeleteAsante tunashukuru kwakutembelea blog yetu endelea kuwa nasi
DeleteDoh, Noma kweli
ReplyDeleteNimeipenda..