Fahamu historia ya kwanini kuliwekwa utambuzi wa alama za vidole(finger print)


Eliezer Gibson 
Katika pita pita zako maeneo fulani bila shaka ulishwahi kukutana na sehemu ambazo walihitaji alama za vidole vyako katika utambuzi wako. au katika matumizi ya simu yako unatumia simu ambayo inahitaji finger print ili kufunguka. Ivi ushawahi jiuliza historia ya kuanzishwa utaratibu huo? Basi kujua hayo tiririka na mimi.


Historia ya alama za vidole(fingerprint) inasemekana ilianzia mnamo mwaka 1858 kwa sir William Herschel mtawala wa kiingereza nchini India. Kutaka alama za vidole zitumike katika kuingia mikataba ya kiserikali.

Lakini stori ya kufurahisha juu ya matumizi ya fingerprint inakuja mwaka 1903,ambako katika gereza moja nchini marekani watu wawili William west na will west walifungwa kwa wakati mmoja lakini wakiingia kwa muda tofauti.

Baada ya william west  wa kwanza kuingia na kusajiliwa kama ulivyo utaratibu wa kawaida. Ikaja muda william west wa pili nae kuingia na kusajiliwa,viongozi wa gereza walikuja kugundua William west wa kwanza pamoja na william west  wa pili wanafanana kwa kila kitu. Kuanzia sura mpaka majina yao japo hawakuwa ndugu.


Baada ya utata huo ndipo gereza hilo lililopo katika mji wa Kansas nchini marekani likaanzisha utaratibu wa kutumia alama za vidole ili kufanya utambuzi wa wafungwa wanaoingia kwenye gereza hilo. Baadaye magerza mengine yalianza kuutumia utaratibu huo wa fingerprints Kama njia ya kutofautisha wafungwa.

No comments