Shahidi wa kesi ya lulu asema 'nilikuta panga chini ya Uvungu siku ya tukio'
Eliezer Gibson


Lulu akiwa mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili
Kesi ya mauji ya bila kukusudia inayomkabilili mwanadada Elizabeth Michael au maarufu Kama lulu.ambaye anadaiwa kumuua bila kukusudia nguli wa filamu za Tanzania marehemu Steven Kanumba mnamo tarehe 7.4.2012 imeendelea leo kwa ushahidi wa tatu kutolewa.
Baada ya jana kutolewa ushahidi kutoka kwa mdogo wa marehemu kanumba,Seth bosco leo ilikua zamu ya daktari na afisa polisi aliyesimamia kesi hiyo ACP Ester zephania kutoa ushahidi wao alianza daktari kisha kumalizia ACP Ester Zephania.
Lulu akiwa mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili
Akitoa ushahidi wake mahakamani hapo.pamoja na mambo mengine Afisa huyo wa polisi alisema alikuta panga chini ya kitanda na michilizi myeusi ukutani wakati alipoenda kufanya upelelezi sehemu ambayo tukio lilitokea.
Kesi hiyo inayovuta hisia za watu wengi inatarajiwa kuendelea kuunguruma 23 October kwa mashahidi wengine kuendelea kutoa ushahidi wao. Ikumbukwe ni miaka mitano imepita tangu tukio hilo kutokea na kuacha simanzi kubwa kwa wananchi wa Tanzania.
No comments