Mjue mwanamke mpigania Uhuru Bi Titi Mohamed
Na Eliezer Gibson


Kama ni mkazi wa Dar es salaam au ama umewahi kufika jijini humo. Bila shaka utakua umewahi kupita au kusikia moja kati ya barabara maarufu jijini humo inaitwa Bibi Titi mohamed road,pengine hujui kwanini inaitwa hilo jina.
Basi kisa cha barabara hiyo kupewa jina la hilo ni kwa ajili ya kumuenzi mmoja ya wanamama mashuhuri katika kupigania uhuru wa Tanganyika bibi Titi mohamed ambaye ni miongoni mwa wanawake wa mwanzo kabisa katika historia ya nchi hii kujikita katika masuala ya siasa na uongozi.
Alizaliwa mwaka 1926 jijini dar es salaam na kufariki mnamo mwaka 2000 mjini johnsberg,South Africa,bibi Titi alianza harakati zake baada ya kukutanishwa na mwalimu Nyerere na mtu anayetajwa kuwa dereva familia yake.
Alishiriki kikamilifu katika kuhakikisha wanawake wanaelewa harakati za uhuru na kushiriki kwa pamoja kupigania haki zao,na pamoja kwa kushirikiana na mwalimu Nyerere na wapigania uhuru wengine walifanikiwa kupata uhuru December 9,1961
Safari ya mwanamama huyo iliingia doa mwaka 1969,ambako yeye na aliyekuwa waziri wa kazi,pamoja na wanajeshi wengine wanne walihukumiwa kifungo cha maisha kwa kile kilochodaiwa kupanga njama za kumpindua rais Nyerere,japo baada ya miaka miwili alipewa msamaha na kurudi uraiani.
Inaelezwa mara baada ya kutoka kifungoni maisha yake yalikua ya tabu,mumewe alimuacha,marafiki zake na washirika wenzake kisiasa walimtenga,hali iliyopelekea kupotea kwenye ulimwengu wa siasa.
Mwaka 1991 katika kushereakea miaka 30 ya Uhuru alitajwa na gazeti la chama cha mapinduzi katika orodha ya mashujaa wapigania uhuru wa Tanganyika,huyo ndiye Bibi Titi mwanamke shujaa mpigania uhuru wa Tanganyika.
No comments