Messi Aungana na Ronaldo kufikisha magoli 100 katika mashindano ya vilabu barani ulaya
Na Eliezer Gibson


Mwanasoka wa kimataifa wa Argentina anayekipiga katika klabu ya Barcelona,Lionel Messi. Jana ameungana na mpinzani wake wa karibu mreno Christiano Ronaldo kufikisha magoli 100 ya mashindano ya vilabu ya UEFA.
Mshindi huyo wa mwanasoka bora wa dunia kwa mara tano,ametimiza magoli hayo mia moja baada ya kucheza mechi 120 katika mashindano tofauti yanayoandaliwa na shirikisho la kabumbu barani Ulaya.
Messi bado yupo nyuma kwa idadi ya magoli dhidi ya Ronaldo,ambaye amekwamisha kimiani magoli 113.baada ya kucheza michezo 151, vilabu vya Manchester,sporting lisbon na Real Madrid.
Ifuatayo ni orodha ya wachezaji waliofunga magoli 50-100 katika mashindano ya ulaya.
No comments