Madrid wachana mikeka,Man city waendeleza moto

Eliezer Gibson

Mechi mbalimbali za ligi kubwa barani ulaya zilipigwa wikiendi hii. Kuanzia nchini England kwenye ligi pendwa mpaka nchini hispania kwa kina ronaldo na messi nyasi ziliumia wakati wanaume wakifanya yao uwanjani,waliotiki mikeka wametiki na waliochana wamechana 



Nchini England vijana wa pep waliendeleza moto walioanza nao kwa ushindi mwembamba dhidi ya westbromwhich Albion ushindi wa 3-2(Sane,sterling na Fernandinho) huku timu za Arsenal 2-1, Man U 1-0, Chelsea 1-0 pamoja na Liverpool 3-0 zote zikiibuka na ushindi.


 Nchini Hispania baada ya juzi usiku lionel messi na Paulinho kuipa ushindi klabu ya Barcelona huku Athletico madrid ikilazimishwa sare ya 1-1. Jana mabingwa watetezi wameshindwa kutamba ugenini mbele ya vijana wapya kwenye Laliga Girona goli la isco halikutosha kuiepusha na kipigo kutoka kwa Girona 2-1.

Matokeo ya wikiendi hii yanaifanya madrid kuwa nafasi ya tatu huku ikiwa nyuma kwa tofauti ya points nane dhidi ya wapinzani wao Barca na Mancity bado wapo kileleni mwa ligi ya Uingereza.

No comments