Breaking news:Nyalandu ajiuzulu Ubunge

Aliyekuwa waziri wa mali asili na utalii katika serikali ya Awamu ya Tano na mbunge wa sasa wa singida kaskzini ametangaza kuhama chama cha mapinduzi.


 Akiandika kupitia akaunti zake za Facebook na Instargram Nyalandu amebainisha kuwa vilevle amemuandikia spika wa bunge la jamuhuri ya Muungano juu ya kujiuzulu kwake nafasi yake ya ubunge.

Mbunge huyo,amebainisha kuwa sababu yake ya kujiuzulu na kujitoa ndani ya chama cha Mapinduzi inatokana na kutorodhishwa kwake na mwenendo wa mambo katika nyanja ya demokrasia na utawala bora hivyo kuona njia pekee ni kujiuzulu na kutokua miongoni mwa wana CCM.

Mbunge huyo ambaye kwa siku za karibuni alionekana kupaza sauti juu ya mambo mbalimbali na kuwa karibu na upinzani,amebainisha adhima yake ya kuhamia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

No comments