Kocha msaidizi wa simba ajiuzulu

Aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya simba Jackson mayanja ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya kocha msaidizi wa klabu hiyo leo hii jijini dar es salaam.




Kocha huyo raia wa Uganda aliyeitumikia Simba kwa misimu mitatu ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia,ambayo yanamlazimu kuwa karibu na familia yake.

Akizungumza na waandishi wa habari na mbele ya msemaji wa klabu hiyo haji manara,Mayanja amesema 'kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia na baada ya kuzungumza na kuelewana na viongozi wa klabu nimeamua kuchukua uamuzi wa kujiuzulu nafasi yangu ya kocha msaidizi'



Bado timu ya simba haijatoa tamko juu ya nani atashika nafasi hiyo ya kocha msaidizi. Iliyoachwa na mganda huyo,klabu ya simba iliyo chini ya mcameron Joseph omog inapigana kunyakua ubingwa wa ligi kuu baada ya kuukosa kwa miaka mitano.

No comments