Mo ASHUSHA KITU KIPYA SIMBA HUKU PANGA LIKIWANYEMELEA WENGI




VELUD YUPO DAR, KUONDOKA NA WENGI

-Klabu ya Simba Sc jana usiku imemshusha kocha mfaransa mwenye uzoefu na soka la Afrika anayejulikana kwa jina la Hubert Velud anakuja kuchukua mikoba ya Joseph Omog aliyetimuliwa December 23 mwaka Jana. Velud  amewahi kuzifundisha vilabu vya  TP Mazembe, Etoille du Sahel na MC Alger.

-Baada ya kuwasili jana alipokelewa na mjumbe mmoja wa kamati tendaji ambaye alipewa maelekezo na  Mohamed Dewji 'Mo' kumpokea. Baada ya kufika Dar anatarajiwa leo kufanya mazungumzo na tajiri huyo pamoja na viongozi wa Simba Sc.

-Habari za kuaminika kutoka Simba Sc zinasema huo ndio mpango wa Mohamed Dewji kuibadili Simba Sc, na Hubert Velud amepewa jukumu la kuleta kocha mwingine mtaaramu wa viungo kutoka nje. Pia Mohamed Dewji 'Mo' anatarajia kushusha kocha mwingine kutoka ulaya ambaye atakuwa kocha wa Timu za Vijana.

-Pia kuhusu Bechi nzima la Simba Sc, Velud atapewa uhuru wa kuamua yeye mwenyewe aendelee na hao waliopo au abadili ila kuna uwezekano wa kubadili bechi la ufundi mwishoni mwa msimu huu.

-Pia Mohamed Dewji 'Mo' anatarajia kushusha mwanadada kutoka Ujerumani kuja kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba Queens, na atakuwa anasaidiwa na watanzania wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.

-Kuhusu Management ya Klabu pia panga litawapitia wengi kinachosubiliwa ni Mohamed Dewji 'Mo' kukabidhiwa timu tu ndio Panga litembee unaambiwa mojawapo ya watu ambao panga litawapitia ni katibu wa Simba, Baadhi ya maafisa wa masoko na wengine huku Haji Manara akipona ila Idara yake itaongezewa watu na kuwa na watu 4. 

From: yossima Sitta Jr.

No comments