BREAKING NEWS: Mama Anna Mghwira atua rasmi CCM
Akihutubia katika mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Mama Anna Mghwira ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi.
Mama Mgwira amesema alikuwa kwenye chama tena mwenyekiti lakini anapenda jinsi chama cha Mapinduzi wanavyopanga mambo yao, yanavyoeleweka ndani ya wanachama na mbele ya umma kwa ujumla.
Amesema akiwa kama mkuu wa mkoa Kilimanjaro anashirikiana na vyama vyote ikiwemo CCM, CHADEMA na NCCR ambavyo ndivyo vyama vikubwa mkoani kwake. Amesema katka vyama vyote, ameona CCM inayobadilika japo anaona juhudi za kila mtu lakini juhudi za mtu anaebadilika huwa ziko tofauti, amesema mtu akiokoka hahami duniani bali anasema amebadilika, anataka kuwa mwema zaidi.
Mghwira amesema anaiona CCM inayoanza kukataa Rushwa, inayotanguliza maslahi ya Taifa mbele na chini ya uongozi wa Jemedari mahiri, Dk John Magufuli hadhani kama kuna mtu atapenda kubaki kwani amerudisha hadhi, heshima ilikuyokuwepo ndani ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Amesema baada ya kufanya kazi chini ya serikali kwa takribani miezi sita ameona ana sababu ya kutangaza anapenda kuungana na chama cha Mapinduzi. Amesema kina mama wana jukumu la kubeba maisha ya watu na sura ya Taifa.
Mama Anna Mgwira amesema anaungana na kina mama wenzake wanaotaka kubadilika, kupambana na kutoa muda wao wa thamani kuhakikisha Taifa linakuwa mahali salama pa kuishi na linakuwa mfano wa kulea jamii kiutu, kizalendo na kiuajibikaji
Source:J.F member
No comments