MICHEZO VYUONI
Ni siku ya Jumatano kama kawaida yetu mpenzi msomaji wa jicho tz tunakusogezea habari ya kimichezo kutoka chuo cha Diplomasia.ambapo leo saa kumi kamili watakua na mchezo mmoja wa kirafiki utakao fanyika uwanja wa Policy Academy maeneo ya ufundi, nilipata bahati ya kuongea na captain wa darasa la Diploma ambaye ni Shaban Sufiani Mwanshuri maarufu kama Justine Realy best nae alisema Anamatumaini makubwa sana kwenye mchezo wa leo, kwasababu kikosi chake chini ya kocha mkuu Kamuzora kimekua na umoja na mshikamano, na kinakila sababu ya kushinda mchezo wa leo dhidi ya darasa la certificate. Aidha ifahamike kwamba diploma wanahistoria nzuri kwenye uwanja huu mara baada ya kuisambalatisha timu ya Diploma 2 mwezi wa tano kwa jumla ya magoli 6-0.
Kwa upande wa certificate wao wanasema Leo ndio siku pekee mtoto hatumwi dukani, watahakikisha wanawafunga mahasimu wao kwa mara ya kwanza.
Makala hii imeandaliwa na mimi mwanamichezo wako HEKELA FESTO KYANDO.

No comments