KILIO CHANGU (MY CRY) Part FOUR



Na
Deo Massawe
MAWASILIANO 0653195298
                    
  "Hiyo mama ina  mkojo,jana usiku nimekojoa kitandani," Miriam aliongea uwongo  ilimradi asije kupoteza namba za Genes,
 "jaman mwanangu mbona ukojoe kitandani jana  akati uliacha kitambo?"mama aliuliza kwa upole,Miriam aliendelea kuwaza kwa nini mama amebadilika na kua mwema kiasi hicho,
 "jana usiku mama ulivyonisukumizia  kidole huku niliumia nahisi ndio maana nilijikuta nakojoa kitandani" Miriam nae alizidisha uongo. Baada ya hapo Miriam alishuhudia gauni lake likianza kusuguliwa tena kwa umakini maana kashadai lina mkojo hivyo mama yake alilifua kwa umakini wa hali ya juu ilimradi asimkwaze tu.
  Miriam nae aliumia sana moyoni kwa kupoteza namba za Genes,
"sasa Genes ataniwaza vibaya, yaani hadi amwagiwe maji machafu kwa ajili yangu alafu nimkatae? hapana" alijisemea moyoni Miriam.
                                 ********
 Genes alikaa na mawazo huku akili yake ikitawala jina Miriam,
"hakika haka kademu kasiponipogia simu nitajua kalinichora tu na kunicheka jinsi nilivyopigwa kofi kubwa na kunyeshwa maji machafu" alijisemea Genes huku akirudisha daftari zake kwenye mkoba kwani alizitoa kwa ajili ya kusoma ila hakuweza kusoma kitu,
"ah kesho acha niwe wa mwisho mimi  siwezi kusoma kichwa changu hakipo" alijisemea Genes kwa kukata tamaa kwani kesho yake jumatatu kulikua na jaribio la  hesabu.
                              ********
 Baada ya mama Miriam kuanika  nguo basi alitoka kutembea nae Miriam alipata nafasi ya kuenda kukagua kwenye lile pindo kama atafanikiwa kuipata  iamba ile, ila hakufanikiwa kwani aliikuta karatasi umekatika vipisipisi, hakua na lakufanya,
"heri huyu mama angeendelea kunitesa tu maana ningefua  nguo zangu mwenyewe" Miriam alijisemea kwa hasira kisha kuanza maandalizi ya kulala kwani tayari ilikua jioni na kama jumatatu huwa ni siku ya kazi hivyo jumapili huwahi kulala.
  Mama Miriam alipunguza tabia ya kulala kwenye starehe,ilimradi akae akimchunga Miriam asije kutana na mwanaume na kumharibia mpango wake,
"angalau saivi huyu mama hatoki  tena usiku kwenda kwenye vikoba maana nilikua muoga kulala mwenyewe ndani" akijisemea Miriam.
                               **********
Baada ya wiki mbili kuisha Genes alishindwa kuvumilia na alitamani kurudi pale kijiweni kwa Miriam lakini aliogopa kipigo,
"labda itakua alipigwa sana na mama yake ndo mana hata kanipotezea,sasa mimi nashindwa hata kusoma mpaka nimuone huyu angalau hata nimsaidie  aweze kupata haki zake kwani pale alipo  anateseka  sana" Genes alijisemea akiwa kujilaza kwenye dawati.
 Mama Miriam siku moja alitoka kwenda kujiuza,kwani kipindi hicho kulitokea ugonjwa wa kipindupindu uliosababisha vubanda vya kuuza vyakula  vifungwe katika nchi nzima  ya Tanzania,
 "kila kitu leo  ni mkosi tupu, yaani nakuja kupigwa na hii baridi yote ya usiku na sipati hata mia? ona watoto wadogo wanavyochukuliwa  na matajiri dah kwangu wanakuja vibaka tu vinauliza kama naonjesha," mama Miriam alijisemea kwa hasira kwani alijipanga barabarani bila mafanikio yoyote hadi akawaza kumleta  Miriam kule,
 "umri wangu huu sasa naona umeenda saivi Miriam akija huku ndio atapata soko, sasa kibanda nimefunga leo  siku ya tatu, kweli njaa itatuua sasa maana mtaji wangu ushakata" mama aliongea hayo akielekea nyumbani kulala hiyo ilikua saa  kumi alfajiri "hebu ngoja nimpigie  huyu dereva anaejiita Faridi nijue anakuja lini maana hali ya maisha inazid kua ngumu na mtoto anazidi kuiva tu" mama Miriam alijisemea huku akinyanyua simu yake mpya aliyoinunua,
"hallo unaongea na mama la  mama hapa"
 "ahaaa nambie mama la  mama, mbona namba tofauti ?"
 "we acha wahuni wa Arusha walinionesha cha moto juzi kati kwenye daladala"
 "ahaa mama pole sana nipe habari"
 "sina habari hata kidogo sema umechelewa kurud bhana na huyu Mtoto wako wakuja kupakata bado nazidi kumnoa kimawazo yaani wewe ukija unakula kilaini sana kama kutafuna big G kwa hiyo jitahid uwahi na uache uhuni wenu madereva wa malori nyie mnafanya sana umalaya,kila mwanamke mnakua mnamtaka hivyo ukichekewa zaid napandisha bei"
"wiki hii mwishoni nakuja mama maana nina hamu kweli, saivi nipo katika barabara moja iliyo katikati ya pori.
 Hayo yalikua maongezi kati ya mama Miriam na dereva Faridi ambae ndie alitoa oda ya bikra ya Miriam. Na kwa mda huo alikua njiani kuelekea mjini Lubumbashi pamoja na utingo wake.
 Katika hilo pori walilokua kulikua na hatari sana kwani makundi mbalimbali ya magaidi yalijificha huko mfano kikundi cha Mai-Mai, M23, hadi Boko haramu kutoka Nigeria.
Makundi hayo yalijikita katika pori hilo kwa ajili ya kuteka  mali kama dhahabu na vyakula  vilivyokua vikisafirishwa katika njia hiyo.
 Utingo nae alikua na furaha ya Kukaribia mda wa kurud nyumbani kwani aliacha mke aliemuoa hata wiki haikuisha akapata safari hiyo basi nae alikua na hamu ya kurudi ili akaendelee na mapenz yakiwa bado ya motomoto nae dereva alikua na furaha kwani alikua anaenda kuonja kitu kwa mara  ya kwanza.
 Kwa umbali dereva aliona magogo yaliyopangwa barabarani akamwambia utingo," itakua magaidi hawa " utingo alitaka kuruka ila dereva akamsihi atulie kwanza,
 " we shuka utoe magogo ndo kazi yako"
 "Hapana suka me ni kuziba pancha" utingo alijibu kwa woga aliogopa kushuka asije  kutekwa,
 Baada ya kubishana kwa mda utingo alishuka na kuanza kutoa magogo ila ghafla dereva aliskia mlio wa risasi na kumuona utingo akiwa kalala  chini akivuja damu kifuani na tayari wakaja watu watatu waliojifunika nyuso  zao dereva akaanza kuhaha  akajua tayar ashatekwa na akajua kifuatacho ni kufa au kuteswa na kukatwa  kichwa kama wanavyofanya  mgambo wa IS (Islamic state).

Usikose kuungana nasi tena hapa hapa jicho tz kwa sehemu ya 5

No comments