ALICHO KISEMA DK.SLAA JUU YA UTEUZI WAKE




Baada ya uteuzi wa Dk.Slaa kuwa gumzo kwenye mitandao leo Hatimaye Aliweza kuhojiwa na moja ya vituo vya habari hapa inchini na kuelezea alivyo pokea uteuzi huo.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Azam, Dkt. Slaa amesema ameona taarifa ya uteuzi kwa njia ya mtandao lakini baada ya muda alitumiwa barua rasmi.

“Ni mapenzi ya Mungu, nashukuru kwa uteuzi. Ninachoweza kusema katika hatua hii, huu ni wajibu mkubwa katika kipindi cha kulijenga taifa letu,” amesema.

Dk Slaa amesema, “Ninachoweza kusema nitakuwa tayari kutoa mchango na mwenyezi Mungu atanisaidia. Ndicho ninachosema kwa hatua hii ya sasa.”

Source: Malunde1

No comments