THOMAS SANKARA (CHE GUEVARA OF AFRICA)
![]() |
Kapteni:THOMAS SANKARA. |
Leo tunawaletea makala ndefu kidogo lakini ni
yakusisimua inayo muhusu shuja wa Burkina Faso Na
Afrika kutokana na sera zake za uongozi huyu ni Kapteni:
Noël Isidore Thomas Sankara.
Au wengi walipenda kumuita Che
Guevara wa Afika.
VIDEO YA MAISHA YAKE bonya hapa=> https://youtu.be/0SACE0PGUbI
THOMAS SANKARA Alizaliwa munamo tarehe 21 Desemba
1949 mjini YAKO,VOLTA
YA JUU. Ambako sasa
kuna julikana kama BURKINA
FASO. (land of upright men). Babake, Joseph Sankara, alikuwa
Msilimi-Mossi Alijipa jina
Ouedraogo alipojiunga na jeshi la UFARANSA wakati wa Vita kuu ya pili ya Dunia. Joseph
alikuwa Muislamu, lakini baada ya kujiunga na jeshi, alibadili dini na akawa
Mkatoliki. Mamake Sankara alikuwa anaitwa Marguerite Kinda, na alikuwa Mmossi. Baada ya Thomas Sankara kufika ujana, babake aliibadilisha jina
ya familia yao tena na wakarudi kuitwa "Sankara". Alipokuwa
mdogo, familia yake iliishi mji wa Gaoua,
kwani hapo ndipo baba yake alipoajiriwa na jeshi. Shuleni, alifuzu katika
masomo ya hisabati, Kifaransa na dini. Kwa kuwa alikuwa mchamungu,
makasisi wake walimshauri aende shule ya seminari baada ya kumaliza shule ya
msingi. Alikubali, lakini pia alifanya mtihani wa kuingia kidato cha sita na
kuipita. Babake alipowajulisha makasisi kwamba Sankara hangekuwa anaenda seminari, bali angejiunga na shule ya
upili, walimjibu kwa kusema hakumwombea mwanake kwa kina.
Sankara
alijiunga na Shule ya Upili ya
Ouezzin Coulibaly, iliyokuwa kule Bobo-Dioulasso.
Huko, alifanya urafiki na vijana wengi ambao baadaye walikuja kuwa wandani wake
alipokuwa serikalini, kama vile Fidele Toe, ambaye akawa waziri, Soumane
Toure, nk. Shuleni, aliendelea
kuyapenda masomo ya Hesabu na Kifaransa, pamoja na kuanza kuigiza kwenye
michezo.
![]() |
Sankara Akipiga gita |
Mwaka wa
1966, rais wa kwanza wa Volta ya Juu, Maurice Yameogo,
aliondolewa kupitia mapinduzi na kamanda wa jeshi,Sangoulee Lamizana. alichukua
uongozi. Lamizana akaanzisha chuo cha wanajeshi mjini Ouagadougou, ambacho kilikuwa cha kwanza nchini. Sankara alisikia kwenye
redio tangazo kwamba wanafunzi wa kwanza wa chuo hicho watachaguliwa kutoka
waliohitimu shule ya upili. Alipohitimu, alikuwa mmoja wa waliochaguliwa.
Wakati huo, alikuwa na umri wa miaka 17.
Baada ya
miaka mitatu, alimaliza masomo yake kwenye chuo hicho cha uanajeshi, na kutumwa Antsirabe, nchini Madagascar.
kusomea cheo cha uafisaa. Huko, alifundishwa na kujifundisha zaidi ya masomo ya
kawaida ya uanajeshi. Masomo ya kilimo, unyunyuzi, na maisha ya raia wa
kawaida. Aliyapenda sana masomo yake huko hadi akaomba ruhusa ya kukaa huko kwa
mwaka mmoja zaidi.
Sankara
alipanda ngazi ya kijeshi hadi cheo cha kapteni
Pamoja na mwanajeshi mwenzake Blaise
Compaore alishiriki katika chama cha siri cha "maafisa Wakomunisti" waliolenga kupambana na ufisadi uliokuwa ukiendeshwa na
watawala..
Mwaka 1981 alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya rais Jean-Baptiste Ouédraogo na kupandishwa cheo kuwa waziri mkuu kwa miezi michache kuanzia
Februari 1983 Mwezi Mei
alikamtawa na kutiwa mbaroni.
Mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Blaise Compaore
yalimfanya kuwa mwenyekiti wa kamati ya mapinduzi na rais wa tano wa Volta ya
Juu.
Baada ya mapinduzi kufanikiwa.Sankara alibadilisha jina la nchi kuwa Burkina Faso. Alijulikana
hasa kwa amri yake ya kuwa
mawaziri na maafisa wote waserikali yake
wasitumie magari makubwa bali gari dogo aina ya Renault
5 ambayo ilikuwa gari la bei ya chini iliyopatikana nchini. Burkina
Faso
Pamoja na
hayo, alishirikisha wanawake wengi katika serikali yake akapiga
marufuku tohara kwa wanawake.
Munamo
tare 15 0kutoba 1987 Sankara ali uwawa na serikari yake kupinduliwa Mapinduzi
ya liyo fanywa na mshilika wake wa karibu ndugu Blaise Compaoré.
ENDELEA
KUFUATILIA MAKALA ZETU KUFAHAMU ZAIDI WATU MAARUFU WALIO PITA KATIKA NYAKATI
TOFAUTI TOFAUTI
KWAMONI
TUANDIKIE
+255758019034.
No comments