Picha ya Tundu lissu yaonyeshwa kwa mara ya kwanza
Baada ya kusubiri kwa zaidi ya siku 40 kuona picha ya mbunge wa singida mashariki na rais wa chama cha wanasheria TLS,hatimaye picha za mbunge huyo zimetolewa akionyesha mwenye afya nzuri
Mbunge huyo aliyepigwa risasi akiwa mjini Dodoma,ambako alikua akishiriki mkutano wa bunge la jamuhuri ya muungano ya Tanzania.kupigwa kwake risasi kulizua taaharuki kubwa miongoni mwa wananchi wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
Kuonekana kwa picha yake akiwa ana tabasamu kunaleta tumaini jipya juu ya afya yake ambayo ilizua hofu miongoni mwa watanzania ambao walihofu pengine angepoteza uhai wake
Akiongea na waandishi wa habari jana,mwenyekiti wa CHADEMA mh Freeman MBowe alibainisha kuwa baada ya kukamilika kwa awamu mbili za matibabu zilizofanyika Tanzania na Kenya,awamu ya tatu ya matibabu itafanyika hivi punde katka nchi ambayo hakuitaja kwa kile alichisema ni sababu za kiusalama.
No comments