AGIZO LA WAZIRI LA SABABISHA KIBOKO KUSHUGULIKIWA.



KUTOKA BUNDA ,MARA:

Siku mbili baada ya Waziri wa kilimo Mh.Charles Tizeba Kutoa agizo kwa afisa  maliasili kijiji cha Nyatwali Bunda mkoa  wa Mara kuuwa  wanyama wote  wanaovamia kijiji hicho na kuharibu mazao ya wananchi agizo hilo  limeanza kutekelezwa baada ya askari wanyamapori kuwaua Viboko  wawili waliovamia kijiji hicho na kuharibu mazao yao

Mwandishi Alifika eneo La tukio na kukuta wananchi hao wakichuna na kugawana nyama hiyo ya kiboko
Wanainchi wa  kimchuna Kiboko


Mwandishi Alizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kwa furaha walipongeza agizo la Mh. Waziri huyo  wa kilimo,kijiji hicho kipo jirani na Mbuga ya Serengeti na wamekuwa wakisumbuliwa na wanyama kama Tembo na Viboko wanaoharibu mazao yao.

PICHA ZAIDI 










#Shukurani kwa MchainaNews.

No comments