UCHANGUZI WA CCM NGAZI YA MKOA-NJOMBE MATOKEO HAYA HAPA
Na: Twalimo Kyando
Njombe.
UCHAGUZI MWENYEKITI WA CCM MKOA NJOMBE Wamalizika
Kwa aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha CCM wilaya ya Makete ndugu mwamwala kuwatupa mbali washindani wenzake katika kinyang'anyiro hicho kwa kupata jumla ya kura za wajumbe 445 na kumwacha ndugu Nicolaus na ndugu Mng'ong'o kwa pamoja wakipata kura 150.
Akizungumzia juu ya ushindi huo mbele ya waandishi wa Habari na wajumbe ndugu mwamwala anasema ataendeleza pale alipoishia mwenyekiti mstaafu mh Deo Sanga maalufu kwajina la (Ja pipo) aliestaafu kwa mujibu wa kanuni mpya za Chama.
Pia anasema atahakikisha anarudisha kata zote zilizochukuliwa na upinzani mwaka 2015 katika uchaguzi. Katika hatua nyingine ndugu Fidelis alichaguliwa kuwa mwakilishi wa mkutano mkuu MNEC Taifa kwa kumshinda mgombea mwenzake ndugu Nyagawa kwa kupata kura 431 dhidi ya 147 za Nyagawa.
Uchaguzi huu unaoendelea unafanywa kwa ngazi za Mkoa na wilaya na baadae mwakani itakuwa ngazi ya taifa pale kizota Dodoma.
No comments