CLOUDS FM YAPIGWA FAINI KWA KOSA HILI...
Serikali kupitia mamlaka ya mawasiliAno nchini (TCRA) imekipiga faini ya shilingi milioni 12 na kukipa onyo kali kituo cha redio cha Cloud FM kwa makosa ya kukiuka maudhui na kanuni za utangazaji.
Cloud FM imekutwa namakosa matatu ambapo kosa la kwanza ni kutangaza habari ya uongo katika kipindi cha Jahazi cha saa 11 Jioni kipengele cha Mastori ya Town na hii imetozwa faini ya Sh. milioni 5.
Pia imetozwa Shilingi milioni 5 nyingine kwa kosa la ukiukaji wa kanuni katika kipengele cha Najua Wajua
Katika kipindi cha XXL, Clouds Fm wametozwa faini ya Sh. milioni 2 kwa kosa la ukiukaji wa kanuni.
Jumla ya faini ni shilingi milioni 12 kwa makosa yote matatu na watatakiwa kuilipa ndani ya siku 30
Pia wamepewa onyo kali na wameaswa kuchukua hatua kali kwa watangazaji wanaokiuka maadili ya utangazaji
Clouds watatakiwa kuomba radhi kwa siku 3 mfululizo kuanzia leo katika kipindi cha jahazi.
ANGALIA VIDEO HAPA CHINI
ANGALIA VIDEO HAPA CHINI
Chanzo cha habari Mtilah blog.
No comments